NI KARIBU WIKI SASA TANGU ALIYEKUWA ASKOFU MKUU, DR MOSES KULOLA KUZIKWA PALE BUGANDO- MWANZA, HAKIKA WANA EAGT NA WAKIRSTO WENGINE BADO WANAOMBOLEZA MSIBA WAKE, HUKU KILA MMOJA AKIENDELEA KUOMBA FARAJA YA MUNGU KWA WAFIWA WA KARIBU; MJANE, WATOTO, NDUGU, MAASKOFU, WACHUNGAJI WA MAKANISA YA EAGT NA WASHIRIKA WOTE KWA UJUMLA.
HAKIKA KAZI YAKE HAPA DUNIANI AMEMALIZA, KILICHO BAKI NI SISI TULIOBAKI KUENDELEA KUSHIKILIA IMANI YETU NA KUTENDA SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU.
KANISA LA EAGT GILGALI MWANJELWA- MBEYA, LINATAZAMIA KUMPOKEA MAKAMU ASKOFU MKUU, DR MWAISABILA AKITOKEA MSIBANI KUREJEA NYUMBANI.
AKITANGAZA KANISANI SIKU YA JUMAPILI, KATIBU WA KANISA NDUGU MBILINYI ALIWAOMBA WAUMINI KUMPOKEA" BABA" NA KUMWOMBEA FARAJA KUTOKA KWA MUNGU KWAKUWA AMETOKA MSIBANI HUKU YEYE AKIWA NI KIONGOZI MKUU MSAIDIZI WA MAREHEMU, NA SASA ANAHITAJI UTULIVU MKUBWA NA KUMWOMBEA SANA ILI MUNGU AMWEZESHE KUFANYA MAJUKUMU YA KULEA NA KUCHUNGA KANISA LOTE LA EAGT.
KWA MJIBU WA KATIBA YA KANISA LA EAGT, MAKAMU ASKOFU ATASHIKIRIA MAJUKUMU YA ASKOFU MKUU HADI HAPO UCHAGUZI UTAKAPOFANYIKA KWA TARATIBU HUSIKA.
ASKOFU ATAFIKA MAJIRA YA MCHANA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SONGWE ULIOKO JIJINI MBEYA, AKITOKEA JIJINI DAR ES SALAAM.
HAKIKA KUREJEA KWAKE INAKUMBUSHA HUZUNI TULIYO NAYO WANA EAGT.
KARIBU BABA, KARIBU ASKOFU, NA MUNGU AKUTIE NGUVU!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni