Jumamosi, 28 Septemba 2013

CHANGIA MIPANGO YA MAENDELEO YA KANISA LA EAGT MWANJELWA

KANISA LA EAGT MWANJELWA CHINI YA MCHUNGAJI, MAKAMU ASKOFU MKUU DR MWAISABILA LINAPENDA KUWASHIRIKISHA WASHIRIKA WA KANISA HILI NA WATU WOTE KWA UJUMLA KATIKA MIPANGO YAKE YA MAENDELEO NA UCHUMI WA KANISA.

LENGO LA IDARA YA MAENDELEO NA UCHUMI KANISANI NI KUTENGENEZA TARATIBU NA MIPANGO ENDELEVU NA YA WAKATI KATIKA KULIFANYA KANISA LA LEO KUWA KITOVU CHA MAENDELEO YA KIROHO NA KIMWILI KWA WAUMINI WAKE NA WATU WOTE (JAMII) KWA UJUMLA. KANISA LINAO UWEZO NA FURSA ZA KUFANIKISHA MAENDELEO KATIKA NYANJA TAJWA.

KANISA LINA MIPANGO MINGI YA KUTOSHA KWA FAIDA YA KANISA, JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA. KWA SASA IDARA YA  MAENDELEO INAENDELEA KURATIBU MICHAKATO MBALIMBALI YA NDANI NA NJE ILI KUHAKIKISHA KUWA MIPANGO ILIYOPO YA MUDA MFUPI NA MREFU INAFANIKIWA. KWA KUSHIRIKIANA NA KAMATI TEULE YA KURATIBU UJENZI WA KANISA;

KWA SASA KANISA LIPO KATIKA MCHAKATO MKUBWA WA UJENZI WA KANISA KUBWA NA LA KISASA KATIKA ENEO LA KANISA. UJENZI HUU UNAKUJA BAADA YA KANISA LA AWALI KUONEKANA HALIKIDHI IDADI YA WASHIRIKA WALIOPO NA KUWA LINA KIWANGO DUNI KWA KUWA LILIJENGWA MIAKA MINGI (1970s).

UJENZI HUU UNATEGEMEA MICHANGO YA WASHIRIKA LAKINI PIA WADAU WA NJE YA KANISA (watu binafsi, taasisi, makampuni na wafanya biashara). HIVYO TUNATOA WITO KWA WADAU (mdau yeyote) KUSHIRIKI PAMOJA NASI KATIKA UJENZI HUU WA KANISA AMBAO HATUA ZAKE ZA AWALI ZIMEKWISHA ANZA.

KUSHIRIKI KWAKO NI BARAKA KWAKO PIA. WAWEZA KUSHIRIKI KWA KUCHANGIA VITU VYA UJENZI KAMA NONDO, BATI, SARUJI, MCHANGA, MAWE nk. LAKINI KWA KUFANYA MAWASILIANO NA KATIBU WA MRADI.

PIA WAWEZA KUSHIRIKI NASI KWA FEDHA TASLIMU KUPITIA MITANDAO YA SIMU (MPESA AU TIGO PESA) AU KULETA MWENYEWE HAPA KANISANI. KUMBUKA KILA KITAKACHO TOLEWA KAMA MCHANGO WA UJENZI HUU UTAPATIWA RISITI.

PIA UNAWEZA KUCHANGIA PESA YOYOTE KUPITIA BANK ACCOUNT: 4263070002 KWA KUANDIKA MAJINA: LYDIA, LUKA, ASUMWISYE & EPHRAIM - BOA BANK MWANJELWA.

KWA MAWASILIANO PIGA:0756 390169

Jumatatu, 16 Septemba 2013

MCHUNGAJI NA MAKAMU ASKOFU MKUU AREJEA NA KUTOA NENO

MCHUNGAJI WETU AREJEA KUTOKA MSIBANI DAR ES SALAAM  NA MWANZA. TUNAMRUDISHIA MUNGU UTUKUFU KWA WEMA WAKE WOTE, KWAKUWA KILA ALIYEHUDHURIA MSIBA ULE ANA MSHUKURU MUNGU KWA KAZI ALIYOFANYA MAREHEMU.

AKIHUBIRI KATIKA IBADA YA JUMAPILI HII, 15/09/2013, MCHUNGAJI AKIRI UZITO WA MSIBA ULE NA KWAMBA HAKIKA MAREHEMU ALIKUWA ASKOFU WA WATU WOTE. 
 PIA ALISISITIZA KUWA JAPOKUWA ASKOFU MKUU HAYUPO TENA, YEYE ATABAKI KUWA MAKAMU ASKOFU MKUU HADI HAPO TARATIBU ZA KIDHEHEBU ZITAKAPOKAMILIKA.

HATA HIVYO ANATAMBUA KUWA KWA WAKATI HUU ATAENDELEA KUFANYA MAJUKUMU YAKE NA YA ASKOFU MKUU, NA KWAMBA SIO VEMA WATU WAKAMVIKA UASKOFU MKUU KABLA YA TARATIBU ZA KIDHEHEBU HAZIJAKAMILIKA.

KATIKA MAHUBIRI YAKE YALIYOSIMAMIA KICHWA CHA UPENDO WA KWELI KIBIBLIA AKISOMA KUTOKA KITABU CHA WAKORINTO WA KWANZA AYA yote YA 13, ALISISITIZA SANA JUU YA WATU WA MUNGU, KANISANI GILIGALI MWANJELWA NA KINGINEKO WOTE KUWA NA UPENDO KAMA ULIVYO NENWA KATIKA BIBLIA, NA KWAMBA KWA KUFANYA HIVYO KUTAKUWA NA AMANI, UMOJA NA BARAKA TELE.

HERI YAO WASIKIAO NENO LA MUNGU NA KULIFANYIA KAZI.

KARIBU KATIKA KANISA LA EAGT MWANJELWA-MBEYA JIJINI.

Jumanne, 10 Septemba 2013

BAADA YA MAZISHI YA ASKOFU MKUU ASKOFU, DR MWAISABILA KURUDI LEO NYUMBANI MBEYA

NI KARIBU WIKI SASA TANGU ALIYEKUWA ASKOFU MKUU, DR MOSES KULOLA KUZIKWA PALE BUGANDO- MWANZA, HAKIKA WANA EAGT NA WAKIRSTO WENGINE BADO WANAOMBOLEZA MSIBA WAKE, HUKU KILA MMOJA AKIENDELEA KUOMBA FARAJA YA MUNGU KWA WAFIWA WA KARIBU; MJANE, WATOTO, NDUGU, MAASKOFU, WACHUNGAJI WA MAKANISA YA EAGT NA WASHIRIKA WOTE KWA UJUMLA.

HAKIKA KAZI  YAKE HAPA DUNIANI AMEMALIZA, KILICHO BAKI NI SISI TULIOBAKI KUENDELEA KUSHIKILIA IMANI YETU NA KUTENDA SAWASAWA NA MAPENZI YA MUNGU.

KANISA LA EAGT GILGALI MWANJELWA- MBEYA, LINATAZAMIA KUMPOKEA MAKAMU ASKOFU MKUU, DR MWAISABILA AKITOKEA MSIBANI KUREJEA NYUMBANI.

AKITANGAZA KANISANI SIKU YA JUMAPILI, KATIBU WA KANISA NDUGU MBILINYI ALIWAOMBA WAUMINI KUMPOKEA" BABA" NA KUMWOMBEA FARAJA KUTOKA KWA MUNGU KWAKUWA AMETOKA MSIBANI HUKU YEYE AKIWA NI KIONGOZI MKUU MSAIDIZI WA MAREHEMU, NA SASA ANAHITAJI UTULIVU MKUBWA NA KUMWOMBEA SANA ILI MUNGU AMWEZESHE KUFANYA MAJUKUMU YA KULEA NA KUCHUNGA KANISA LOTE LA EAGT.

KWA MJIBU WA KATIBA YA KANISA LA EAGT, MAKAMU ASKOFU ATASHIKIRIA MAJUKUMU YA ASKOFU MKUU HADI HAPO UCHAGUZI UTAKAPOFANYIKA KWA TARATIBU HUSIKA.

ASKOFU ATAFIKA MAJIRA YA MCHANA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA SONGWE ULIOKO JIJINI MBEYA, AKITOKEA JIJINI DAR ES SALAAM.

HAKIKA KUREJEA KWAKE INAKUMBUSHA HUZUNI TULIYO NAYO WANA EAGT.

KARIBU BABA, KARIBU ASKOFU, NA MUNGU AKUTIE NGUVU!