MCHUNGAJI WETU AREJEA KUTOKA MSIBANI DAR ES SALAAM NA MWANZA. TUNAMRUDISHIA MUNGU UTUKUFU KWA WEMA WAKE WOTE, KWAKUWA KILA ALIYEHUDHURIA MSIBA ULE ANA MSHUKURU MUNGU KWA KAZI ALIYOFANYA MAREHEMU.
AKIHUBIRI KATIKA IBADA YA JUMAPILI HII, 15/09/2013, MCHUNGAJI AKIRI UZITO WA MSIBA ULE NA KWAMBA HAKIKA MAREHEMU ALIKUWA ASKOFU WA WATU WOTE.
PIA ALISISITIZA KUWA JAPOKUWA ASKOFU MKUU HAYUPO TENA, YEYE ATABAKI KUWA MAKAMU ASKOFU MKUU HADI HAPO TARATIBU ZA KIDHEHEBU ZITAKAPOKAMILIKA.
HATA HIVYO ANATAMBUA KUWA KWA WAKATI HUU ATAENDELEA KUFANYA MAJUKUMU YAKE NA YA ASKOFU MKUU, NA KWAMBA SIO VEMA WATU WAKAMVIKA UASKOFU MKUU KABLA YA TARATIBU ZA KIDHEHEBU HAZIJAKAMILIKA.
KATIKA MAHUBIRI YAKE YALIYOSIMAMIA KICHWA CHA UPENDO WA KWELI KIBIBLIA AKISOMA KUTOKA KITABU CHA WAKORINTO WA KWANZA AYA yote YA 13, ALISISITIZA SANA JUU YA WATU WA MUNGU, KANISANI GILIGALI MWANJELWA NA KINGINEKO WOTE KUWA NA UPENDO KAMA ULIVYO NENWA KATIKA BIBLIA, NA KWAMBA KWA KUFANYA HIVYO KUTAKUWA NA AMANI, UMOJA NA BARAKA TELE.
HERI YAO WASIKIAO NENO LA MUNGU NA KULIFANYIA KAZI.
KARIBU KATIKA KANISA LA EAGT MWANJELWA-MBEYA JIJINI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni