IDARA/KAMATI YA MAENDELEO NA UCHUMI

KANISA LA EAGT GILIGALI MWANJELWA, chini ya Askofu, Dr Asumwise Mwaisabila ni moja ya makanisa makubwa chini ya dhehebu la Evangelistic Assemblies of God (Tanzania) chini ya Askofu mkuu Moses Kulola. 

Ni dhahiri kuwa Kanisa ni taasisi kama zilivyo taasisi nyingine, tofauti yake ni malengo makuu, na kwamba kanisa la mahali pamoja linaingia katika kundi la taasisi za dini (Faith based organizations).

Hivyo kama taasisi yenye uongozi, watu na rasilimali linahitaji kuwa na mipango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kwa upande mmoja, makanisa mengi hasa ya kiroho yameegemea zaidi katika masuala ya kiroho na kwa kiasi kidogo masuala ya kijamii. 

Kwa Upande wa masuala ya maendeleo ya kiuchumi hali bado iko nyuma. Hivyo DHANA ya maendeleo katika makanisa haya, bado haijachukuliwa umuhimu mkubwa.

Kanisa la EAGT GILIGALI MWANJELWA MBEYA chini ya Askofu na mchungaji Dr Mwaisabila, limeanza KUTAFSIRI dhana hii na tayari kama Kanisa, limeunda KAMATI/ADARA ya MAENDELEO na UCHUMI ambayo itashughulikia mipango yote ya maendeleo ya kanisa kiroho, kijamii na kiuchumi.

Ni dhahiri kuwa mipango hii inahitaji kuratibiwa na kutekelezwa KIMKAKATI kwa kuwa kila mpango wa maendeleo ni mchakato. Kwa kuanza, Kamati ya Maendeleo na Uchumi ikishirikiana na mshauri mwelekezi wa masuala ya uchumi na miradi, Mr Miki Kihega, imeandaa MPANGO MKAKATI WA MAENDELEO wa kanisa hili ambao umeainisha miradi yote yenye uelekeo wa kusaidia Kanisa, waumini wake, jamii na taifa kwa ujumla. 

Ni dhamira ya Kanisa hili kupitia idara hii kuona kuwa HUDUMA MAMA zake ambazo ni za kiroho (Maombi, maombezi, ibada za neno, ibada za kusaidia wenye uhitaji, ibada za sifa na kuabudu, uinjilisti nk) zinapata msukumo wa kipekee katika kanisa na nje ya kanisa. 

Kamati hii inatoa WITO kwa waumini wote kushikamana pamoja ili mipango hii ilete TIJA za kiroho na kimwili na hatimaye kuleta mtazamo mpya ambao ni chanya mbele ya jamii na wadau wengine. 

Pia kwa yeyote asiye mshirika/muumini wa kanisa hili anakaribishwa kufuatilia mipango yetu na hakika Mungu atambariki kwa hilo. Kwa sasa MPANGO mkubwa unao endelea kimchakato ni UJENZI WA KANISA KUBWA hapahapa katika eneo la KANISA na Mpango wa KUANZISHA KITUO CHA UFUNDI MCHANGANYIKO- Uashi, uselemala, ushonaji, umeme na umakenika.

 KARIBUNI WOTE EAGT GILIGALI MWANJELWA- MBEYA... MUNGU AWABARIKI. 

 MAWASILIANO: Katibu wa kamati 0754394003

Maoni 2 :