HATIMAYE ALIYEKUWA MAKAMU ASKOFU MKUU WA EAGT, DR. REV ASUMWISYE MWAISABILA AWA ASKOFU MKUU.
NI HONGERA NA BARAKA KWA WANA EAGT WOTE, KWAKUWA SASA WAMEPATA KIONGOZI MKUU WA DHEHEBU LAO, BAADA YA ALIYEKUWA KIONGOZI MKUU DR MOSES KULOLA KUTWALIWA NA MUNGU MIEZI MICHACHE ILIYOPITA.
KANISA LA EAGT MWANJELWA MBEYA, WANAYO SHUKRANI KUBWA SANA MBELE ZA MUNGU KWAKUWA ASKOFU MKUU HUYU NDIYE MCHUNGAJI WA KANISA HILI. HIVYO KWAO NI BARAKA ZAIDI NA ZAIDI.
ANGALIZO NI KWAMBA WANA EAGT MWANJELWA WANATAKIWA KUTAMBUA KUWA SASA MCHUNGAJI WAO NI MCHUNGAJI WA WASHIRIKA WOTE WA EAGT TANZANIA NA WAPENTEKOSTE WOTE KWA UJUMLA.
AKIHUBIRI KATIKA IBADA YA LEO; 17/11/2013 MWINJILISTI ERENEST LWEHABURA AMEWATAKA WANA EAGT MWANJELWA KUMPA USHIRIKIANO ASKOFU MKUU KWA KUWA ATAKUWA AKIFANYA MAJUKUMU YAKE AKITOKEA KATIKA KANISA HILI, HIVYO WASHIRIKA WAKIMPA SAPOTI KUBWA ATAWEZA KUFANYA KAZI ZAKE VEMA KWA FAIDA YA EAGT TAIFA NA WATANZANIA KWA UJUMLA.
MUNGU AMBARIKI NA KUMLINDA BABA YETU, AVAE HEKIMA ZITOKAZO KWA MUNGU NA UCHAJI WA HALI YA JUU WA KIMUNGU.