Alhamisi, 29 Agosti 2013

BWANA AMETWAA NA BWANA AMETOA JINALAKE LIBARIKIWE PUMZIKA BISHOP MOSES KULOLA.

Nihuzuni ndani ya kanisa la Eagt kwa kumpoteza muasisi wa kanisa letu,hatuna la kusema zaidi ya kumpa mungu utukufu kwa yote yaliyo tukia.

                                           Enzi za uhai wake akiwa anahubiri.


Jumapili, 18 Agosti 2013

BAADA YA MKUTANO WA NJE, KARIBU KATIKA SEMINA YA NENO LA MUN

BAADA YA MKUTANO WA NJE KUFANA SANA, SASA NI ZAMU YA KUPATA MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU ILI KUKUA KIROHO. KANISA LIMEANDAA SEMINA NZURI YA NENO LA MUNGU ITAKAYO FANYIKA NDANI YA KANISA.

SEMINA HII YA BARAKA ITAKUWA NA UPAKO WA KIPEKEE KWANI ITAFANYWA NA MWALIMU WA NENO LA MUNGU KUTOKA KANISA LA EAGT-TEMEKE-DAR ES SALAAM.

SEMINA ITAANZA TAREHE 19/08/2013 HADI 24/08/2013 KUANZIA SAA 10.00 JIONI.

WATU WOTE MNAKARIBISHWA, MSISITIZO PIA UKIWA KWA WOTE WALIO OKOKA KATIKA SIKU ZA  MKUTANO NA WASHIRIKA WOTE.



SEHEMU YA MKUTANO SIKU YA MWISHO

HAKIKA MKUTANO WA INJILI KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA EAGT  GILIGALI MWANJELWA-MBEYA UMEFANA SANA NA UMEKUWA WA BARAKA, UPONYAJI NA WENGI WAMEOKOKA.

HAPA NI SEHEMU TU YA WANAMKUTANO KATIKA VIWANJA HIVI.








TUTAWALETEA PICHA ZAIDI ZA MKUTANO HUU, ILI KUNIONEA JINSI YESU ALIVYO WAHUDUMIA WATU WAKE, KUPITIA MHUBIRI DR DANIEL MOSES KULOLA.

Ijumaa, 16 Agosti 2013

KARIBU KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI

TANGAZO LA MKUTANO WA INJILI

ASKOFU, MCHUNGAJI, DR MWAISABILA ANAWATANGAZIA WATU WOTE KUWA KUANZIA TAREHE 14/08/2013 HADI 18/08/2013 KUTAKUWA NA MKUTANO MKUBWA WA INJILI KATIKA VIWANJA VYA KANISA LA EAGT GILIGALI MWANJELWA.

MHUBIRI WA MKUTANO HUO NI MWINJILISTI DANIEL KULOLA KUTOKA MWANZA.

KWAYA NA WAIMBAJI  MBALIMBALI WATAHUDUMU. WALETE WAGONJWA NA WENYE SHIDA MBALIMBALI MHUBIRI ATAWAOMBEA.

NI WAKATI WA MUNGU KUVUNA WALIO WAKE.

KANISA LIPO SOWETO, KM 1 KUTOKA KITUO CHA BASI CHA SOWETO, BARABARA YA LAMI KUELEKEA SHUKRANI CENTRE, KARIBU NA UKUMBI WA MTENDA.

KARIBU WOTE, MKARIBISHE NA MWENZIO!!

KWA MAWASILIANO: 0756390169